Baada ya uzoefu mkubwa katika
matumizi ya mapishi jikoni, ungo umejizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingizwa rasmi katika tasnia ya
sanaa hususani katika ubunifu wa mavazi na
kupewa jina la LUPAHERO na Jocktan Makeke.
Maana ya LUPAHERO
Ubunifu huu wa mavazi umepewa
jina la LUPAHERO ambalo ni mchanganyiko wa majina mawili ambayo ni LUPAPIKE, neno
la kinyakyusa lenye maana ya ungo na neno la pili ni LUHELO, ambalo ni neno la
kihehe lenye maana ya ungo.
Muunganiko wa maneno haya mawili
umelenga kuleta dhana ya ushujaa kutokana na ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima
hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi za mwisho kama Hero, herufi L ikibadilishwa
kuwa R ili kupata neno hero la kingereza lenye maana ya shujaa na kukamilisha
maana halisi ya ubunifu huo kuwa shujaa wa ungo.
Jinsi wazo lilivyopatikana
Katika maandalizi ya onyesho la
kwanza kufanywa chini ya MAKEKE INTERNATIONAL lililofahamika kama I AM MAKEKE
ndipo wazo hili la lupahero
lilipozaliwa. Kwa mujibu wa MAKEKE INTERNATIONAL ilimchukua mudamrefu kupata
wazo la kufanya katika onyesho hilo licha ya kua na bidhaa nyingi za kubuni
nguo mbali mbali ofisini kwake.
Baada ya kuwaza kwa muda mrefu
ndani ya ofisi alitoka nje na kurudi baada ya kutuliza akili lakini wakati
akirudi aliuona ungo kupitia dirisha uliokua umetundikwa ukutani kama pambo la
ofisi ambapo aliamua kuuchukua na kukaa nao huku kichwa kikiendelea kuwaza na
kuwazua ni wazo gani ataonyesha kwenye onyesho lililokua mbele yake.
Baada ya kuwaza kwa masaa kadhaa
wazo lilimjia na kutaka kutoboa ungo aliokua nao kwa kiasi cha kuweza kuvaa
shingoni ambapo alifanya hivyo na kupata ladha ya mapambo ya shingoni ya
kimasai ila katika mwonekano wa ungo na ndopo alipoanza kufikiria mikato
mingine ambayo ungo unaweza kuingia na kudhihirisha ubunifu wa ungo kama vazi.
Baada ya kupata yote hayo makeke
alichukua daftari na kuanza kuchora kila alichokua amekiwaza kwa ufanisi zasidi
na kufanyia kazi kwa muda aliokua nao hali iliyofanya ubunifu wa ungo kutumika
kwa mara ya kwanza katika tamasha la I AM MAKEKE mpaka hivi sasa.
Mikato ya Lupahero
Hapa zitakaa picha za mikato ya ungo kama ya shingoni, mikononi
mgongoni kifuani nakadhalika
MAKEKE INTERNATIONAL imelenga
zaidi kujenga dhana ya ushujaa na asili ya kiafrika ili kujenga mazingira ya
kuweza kujiamini na kujua kuwa wewe ni bora zaidi kutokana na jinsu ulivyo kama
mwafrika na shujaa kwa kila jambo.
About
Makeke International
Get to know JOCKTAN MAKEKE @makeke_international
is an award-winning costuming artist whose design ideas have an African culture content and theme. Jocktan has been a self-taught artist from his childhood; much of what
he has learned has come from interaction and observation of other great artists
Jocktan became fascinated with painting, drawing and fashion designing and so it was only natural that in 2009 Jocktan joined University of Dodoma, College of Arts Media and Design
(A.M.D.) where he received a BA, In Fine arts & Design in 2012.
Related Posts